Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inawashikilia watu wanne kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), jijini Dar es Salaam, James Temba.                                     

Mwili wa Temba ambaye ni mkazi wa Tabata Chang’ombe jijini Dar es Salaam ulikutwa ukielea kwenye maji yaliyokuwa yanatiririka Mto Msimbazi eneo la Kipawa Ilala Aprili 30, 2026 huku ukiwa hauna kichwa.

Wakati mwili wa Temba leo Jumatano, Mei 6, 2026 ukiagwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Tabata Magengeni kisha kusafirishwa kwenda Moshi mkoani Kilimanjaro Kijiji cha Telamande kwa maziko kesho Alhamisi, Polisi wametoa taarifa zaidi juu ya tukio hilo.

Taarifa ya Polisi imewataja wanaoshikiliwa ni Steven Chaka (31), ofisa maabara Mkazi wa Bomang’ombe, Wilaya ya Hai, Kilimanjaro. Mwingine ni Anna Lema (30), Mkazi wa Mkazi wa Tabata Chang’ombe ambaye pia ni mfanyabiashara.

Wengine ni Twalibu Khamis (23), mkazi wa Kigogo Kati na Michael John (26), mkazi wa Kigogo Kati.

“Vipo pia baadhi ya vielelezo ambavyo vinachunguzwa kuhusiana na tukio hilo. Wito wa Jeshi la Polisi kwa wananchi ni kuwa watulivu ili kila aliyehusika kulingana na ushahidi aweze kuchukuliwa hatua za kisheria,” imeeleza taarifa hiyo ya polisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *