Rais wa DRC, Felix Tshiesekedi, katika hotuba yake kwa taifa, ameonesha uwezekano wa kutaka kuongoza kwa muhula watatu pamoja na kuchelewesha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika baada ya miaka miwili.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tshisekedi ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2019 ambapo muhula wake wa pili unatamatika mwaka 2028, amesema hajaomba kugombea kwa muhula watatu, lakini ikiwa wananchi watamtaka afanye hivyo atakubali.

Aidha Tshisekedi alizungumzia uwezekano wa kusongeza mbele uchaguzi wa mwaka 2028, akisema ikiwa vita mashariki mwa nchi haitamalizika karibuni, haoni kama nchi itaweza kuandaa uchaguzi huru na wakuaminika.

“Ningefurahi kumaliza mihula yangu miwili nikiiacha nchi hii katika njia sahihi, hasa kwa kuiacha iwe na amani, lakini ikiwa watu wa Kongo wataniomba niendelee, niko mikononi mwao mradi tu Mungu anipe nguvu inayohitajika.” Alisema Rais Tshisekedi.

Hata hivyo kwa wachambuzi wa mambo wanasema mpango wowote wa kurekebisha katiba hautakuwa na afya kwa demokrasia ya nchi hiyo.

Kufuatia kauli yake, upinzani nchini humo umeendelea kusisitiza kuwa utapinga kwa nguvu zote mpango wowote wa mabadiliko ya katiba, wakimtuhumu rais Tshiesekedi kwa kujaribu kubakia madarakani kupitia kile walichokitaja kuwa ni mlango wa nyuma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *