
Jeshi la Marekani linadai kuishambulia Iran baada ya shambulio dhidi ya meli zake kadhaa. Kwa upande wake, Iran inasema imerusha makombora siku ya Alhamisi, Mei 7, “baada ya jeshi la Marekani kushambulia meli ya mafuta ya Iran” na inaishutumu Marekani kwa kuvunja makubaliano ya kusitisha mapigano.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Iran inadai kufyatua makombora siku ya Alhamisi, Mei 7, “baada ya jeshi la Marekani kushambulia meli ya mafuta ya Iran” na inaishutumu Marekani kwa kuvunja makubaliano ya kusitisha mapigano. Kwa upande wake, jeshi la Marekani linadai kuishambulia Iran baada ya shambulio dhidi ya meli zake kadhaa. Donald Trump anasisitiza kwamba makubaliano ya kusitisha mapigano bado yanaendelea.
Hali imeripotiwa kuwa tulivu katika Mlango wa Hormuz
Kulingana na kituo cha habari cha Iran, kufuatia urushianaji risasi kati ya vikosi vya majini vya Marekani na Iran, hali karibu na Mlango wa Hormuz imerejea katika hali ya kawaida.
Wakati huo huo Marekani na mataifa ya Ghuba yametoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuitaka Iran iache kuzuia urambazaji katika Mlango-Bahari wa Hormuz, wakati rasimu ya azimio linalohusu hilo ikitishiwa na Urusi kwa kura ya turufu.