
Jeshi la Iran (IRGC) limetishia kulenga maeneo ya Marekani iwapo meli za mafuta za Iran zitashambuliwa, huku Washington ikiwa bado inasubiri majibu ya Tehran kuhusu pendekezo lake la hivi karibuni la mazungumzo.
Katika taarifa iliyotolewa hapo
jana, siku moja tu
baada ya Marekani kushambulia meli mbili za mafuta za Iran katika Ghuba ya
Oman, Iran imesema
kwamba “shambulio lolote dhidi ya meli za mafuta na meli za kibiashara za Iran, zitawafanya washambulie vituo vya
kijeshi vya Marekani Pamoja na meli za adui”