Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano kati ya Ufaransa na Afrika uliokamilika jioni hii jijini Nairobi nchini Kenya, wamehoji kuachwa kwa masuala muhimu wanayosema hayakupewa kipaumbele katika mkutano huo wa siku mbili.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kutohudhuria kwa wakuu wa nchi zinazoongozwa na jeshi kutoka ukanda wa Afrika Magharibi, ambazo uhusiano wao na Nigeria umeyumba, kumeonekana kuligawa bara Afrika kwa wawakilishi wa nchi hizo kutoonekana kwenye mkutano wa Nairobi.

Fabrice Muchinga mtaalam wa masuala ya siasa, amani na usalama aliyehudhuria mkutano huu, anaona Ufaransa imekutana na rafiki zake na sio Afrika.

Huu ni mkutano kati ya Ufaransa na rafiki zake, kutoonekana kwa nchi kama za Mali, Burkina Faso na Niger, kunaonesha kuwa bara la Afrika limegawanyika.” Amesema Fabrice Muchinga.

Mataifa ya Niger, Mali na Burkina Faso yaliokuwa koloni ya Ufaransa hayakuhudhuria mkutano wa Ufaransa na Afrika jijini Nairobi.
Mataifa ya Niger, Mali na Burkina Faso yaliokuwa koloni ya Ufaransa hayakuhudhuria mkutano wa Ufaransa na Afrika jijini Nairobi. REUTERS – Thomas Mukoya

Wito wa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Mohammed Ali Youssouf, kuwa changamoto za kiusalama barani Afrika hazipaswi kukwamisha maendeleo ya kiuchumi, wajumbe kutoka DRC wanaona kuwa suala la utovu wa usalama katika nchi yao, linapaswa kupewa kipaumbele.

“Tunatamani mikutano kama hii, isaidie kurejesha amani kwenye nchi yetu, wanawake na watoto wanateseka sana. Watu wanaendelea kuuawa kila siku-Amesema Safi Kahozi, mmoja wa wajumbe kutoka DRC.” Mmoja wa wajumbe kutoka DRC.

Mkutano wa siku mbili kati ya Ufaransa na Afrika umekamilika jijini Nairobi.
Mkutano wa siku mbili kati ya Ufaransa na Afrika umekamilika jijini Nairobi. REUTERS – Monicah Mwangi

Kukamilika kwa mkutano wa mataifa ya Afrika na nchi ya Ufaransa, haukuwa tu wa kibiahara bali pia kiusalama na kisiasa, mambo muhimu yanayohitajika kwenye uwekezaji.

Victor Abuso, KICC Nairobi, RFI Kiswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *