Katibu wa NEC Itikadi uenezi na mafunzo wa chama cha mapinduzi (CCM)Taifa Kenani Kihongosi amewataka viongozi wa serikali kuenzi naono ya baba wa taifa Hayati Mwalimu Julisua Kambarage Nyerere kwa kufanya kazi kwa weledi na kuacha kiburi wakati wakiwatumikia wananchi.

Kihongosi ametoa kauli hiyo leo Mei 15/2026 alipozuru na kufanya ibada fupi katika kaburi la baba wa taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wilaya ya Butiama Mkoani Mara akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2025-2030 mkononi humo.

Amesema falsafa ya Mwalimu Nyerere ilijielekeza kwenye utu,amani,umoja,haki na usawa ambapo alikataa udini,ukanda na ukabila,Mpaka leo mchango na heshima yake bado unaheshimkwa na mataifa mbalimbali na kumsifu Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa anaishi maono ya Mwalimu Nyerere kwa namna anavyowatumikoa watanzania

Amesema viongozi wanatakiwa kuishi na kutekeleza majukumu yao kwa kufuata misingi iliyoasisiwa na Mwalimu Nyerere badala ya kuwa na kiburi cha madaraka bila

Amesisitiza kuwa Chama cha Mapinduzi kitaendeela kuenzi na kusimamia misingi ya haki,usawa na utawala bora iliyoasisiwa na baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *