Viongozi wa kidini wamesisitizwa kufata utaratibu wa kupata Reseni za kufungisha ndoa kwa waumini wao ikiwa ni sehemu ya kukidhi matakwa ya sheria juu ya ufungishaji wa ndoa.
Wakili serkali kutoka RITA Nyanda Masunga ametoa msisitizo huo kwa viongozi wadini kutokana na uwepo wa baadhi ya viongozi hao kutoa vyeti vya kidini kwa waumni wao baada ya uwafungisha ndoa hali inayosababisha ndoa hizo kutotambulika kisheria.
Amesema kuwa mwenye jukumu la kuhakikisha ndoa imesajiliwa ni viongozi wa dini kwa kuhakikisha wanapata leseni za kufungisha ndoa ili weweze kutoa vyeti vya ndoa vya kiserikali kutoka wakala wa usajili ufilisi na udhamini RITA.
Wakishirikiana na wataalamu kutoka Wizara ya Katiba na Sharia katika kampeni ya Mama Samia Legal Aid mkoani Shinyanga wakala wa usajili, ufilisi na udhamini RITA wamesema taasisi hiyo pia inajihusha na usajili wa ndoa na talaka,usajili wa bodi ya uzamini na masuala ya mirathi na wosia.
(Feed generated with FetchRSS)