
Duru ya tatu ya mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Israel na Lebanon yameanza mjini Washingtonsiku ya Alhamisi, siku chache kabla ya kumalizika kwa makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo yalipunguza uhasama lakini hayakuzuia mapigano kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Lebanon Hezbollah.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Maafisa wa Lebanon wanatumai kwamba mazungumzo hayo ya siku mbili yataza marunda mazuri kwa kufikia makubaliano mapya ya kusitisha mapigano na kufungua njia ya kukabiliana na mfululizo wa masuala magumu, ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwa vikosi vya Israel kutoka kusini mwa Lebanon na kupokonya silaha Hezbollah.
Utawala wa Trump umekuwa ukishinikiza mafanikio kati ya majirani hao wawili ambao wamekuwa katika hali ya vita rasmi tangu taifa la Israel lilipoanzishwa mwaka wa 1948.
Hata hivyo, Hezbollah si sehemu ya mazungumzo hayo na imekuwa ikipinga vikali Lebanon kushiriki katika mazungumzo ya moja kwa moja na Israel.
Israel na kundi la wanamgambo linaloungwa mkono na Iran wameendelea kkurushiana risasi karibu mara kwa mara kuvuka mpaka licha ya usitishwaji mapigano kuanzishwa na Marekani Aprili 17. Hapo awali makubaliano ya kusitisha mapigano ya siku 10, kisha yakaongezwa kwa wiki nyingine tatu.
Mazungumzo yanaelekea ngazi ya juu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, ambaye alihudhuria mikutano ya kwanza ya Israel na Lebanon huko Washington mwezi Aprili, alikuwa na Rais Donald Trump katika ziara nchini China na hakuhudhuria kikao cha Alhamisi.
Duru ya sasa ya mazungumzo inawakilisha hatua kuelekea mazungumzo mazito zaidi, huku wajumbe wa ngazi ya juu kutoka Lebanon na Israel wakishiriki baada ya vikao vya awali vya maandalizi kuongozwa na mabalozi wa nchi hizo mbili huko Washington.
Mjumbe wa Lebanon anayeongoza mazungumzo ya Alhamisi, Simon Karam, ni wakili na balozi wa zamani wa Lebanon nchini Marekani ambaye hivi karibuni aliiwakilisha Lebanon katika mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Israel kuhusu utekelezaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyotangulia kuzuka kwa vita hivi karibuni kati ya Israel na Hezbollah. Kwa upande wa Israel, Naibu Mshauri wa Usalama wa Taifa Yossi Draznin alitarajiwa kuhudhuria.
Bado kuna mapengo makubwa katika kile ambacho pande hizo mbili zinakitaka kutoka kwa mazungumzo ya moja kwa moja. Maafisa wa Israel wamejikita katika kuipokonya silaha Hezbollah na kuelezea mazungumzo hayo kama kitangulizi cha uwezekano wa kurasimisha uhusiano wa kidiplomasia. Maafisa wa Lebanon wamesema wanatafuta makubaliano ya usalama au usitishaji vita ambao ungezuia kurasimisha vita.
Trump ameitisha hadharani mkutano kati ya Rais wa Lebanon Joseph Aoun na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, huku Aoun akikataa kukutana au kuzungumza moja kwa moja na Netanyahu katika hatua hii – hatua ambayo inaweza kusababisha mzozo nchini Lebanon.