Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Kinondoni imefanikiwa kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali zaidi ya Shilingi Milioni 500 katika kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu baada ya kufuatilia baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa hawalipi mapato hayo.
Naibu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kinondoni, Elizabeth Mokiwa amesema udhibiti huo umefanyika baada ya kupokea taarifa za kuwepo kwa baadhi ya wafanyabiashara wasiolipa ushuru wa huduma (Service Levy) unaotozwa kwa wafanyabiashara kulingana na mauzo yao ya mwaka kwa mujibu wa sheria ya fedha za serikali za mitaa sura 290.
Mhariri @moseskwindi
(Feed generated with FetchRSS)