Nchini Mali, waasi wa Azawad Liberation Front, wanaotaka kujitawala Kaskazini mwa nchi hiyo, wanasema wanawashikilia wanajeshi zaidi ya 200 kama wafungwa wa kivita katika mji wa Kidal.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tangazo la waasi hawa linakuja, baada ya kudhibiti mji wa Kidal kufuatia mashambulizi makubwa waliyotekeleza pamoja na wanajihadi wa JNIM, Aprili 25.

Waasi hao wameonesha mkanda wa video, ukiwaonesha wanajeshi hao waliovalia mavazi ya raia, na kueleza kuwa wengine walitoroka baada ya mji wa Kidal kuanguka mikononi mwao.

Aidha, waasi hao wamesema wanajeshi hao wa Mali wanangaliwa vizuri, na wametoa wito kwa mashirika ya Kimataifa kuwatembelea ili kuthibitisha hilo.

Wakati hayo yakijiri, nalo jeshi la Mali limeendeleza mashambulizi ya angaa katika mji wa Kidal kuwalenga waasi hao, operesheni wanaosema itaendelea katika siku zijazo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *