Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo na bilionea wa Nigeria na mwanzilishi wa Dangote Group, Aliko Dangote katika Ikulu jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadili mpango wa uwekezaji wa kiwanda kikubwa cha kuchakata mafuta katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Dangote amesema kiwanda hicho kinatarajiwa kuchakata mapipa 650,000 ya mafuta kwa siku, huku eneo la ujenzi bado likiwa halijaamuliwa baada ya wataalamu kupewa jukumu la kufanya tathmini.
Dangote amesema serikali za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zitakuwa sehemu ya wamiliki wa mradi huo, huku akieleza matumaini ya utekelezaji kuanza mwaka huu.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)
