Comoro: Serikali yasitisha ongezeko la bei ya mafuta baada ya madereva na wafanyabiashara kugomaComoro: Serikali yasitisha ongezeko la bei ya mafuta baada ya madereva na wafanyabiashara kugoma

Nchini Comoro, serikali imerejelea hatua yake na kusitisha kupanda kwa bei ya mafuta baada ya mgomo wa siku sita uliosababisha vifo vya watu wawili na kusababisha mvutano katika visiwa hivyo. Tangazo hilo lilitolewa siku ya Jumamosi jioni mbele ya wawakilishi wa vyama vya usafiri na wafanyakazi. Tangu kuanza kwa mgomo huo siku ya Jumatatu, Mei 11, vizuizi vya barabarani, makabiliano, na kuzorota kwa shughli za kuchumi vimeikumba nchi hiyo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Moroni, Abdallah Mzembaba

Katika taarifa yake, serikali imetangaza kusitishwa kwa muda kwa amri zinazoongeza bei ya mafuta na uzinduzi ujao wa mashauriano ya kitaifa na wadau husika. Mamlaka inatumai kuanza tena kwa shughuli za usafiri na biashara mapema leo Jumapili, Mei 17, 2026. Wito ambao vyama vya wafanyakazi vimesema viko tayari kutikia.

Tangu mwanzo wa mgogoro huo, shughuli za kiuchumi zimezorota, haswa huko Moroni. Maeneo kadhaa kote nchini yalikumbwa na makabiliano kati ya vijana na vikosi vya usalama katika siku za hivi karibuni.

Uchunguzi waanzishwa baada ya makabiliano makali

Huko Anjouan, ofisi ya mwendesha mashtaka ya Mutsamudu imefungua uchunguzi kufuatia makabiliano kati ya waandamanaji vijana na vikosi vya usalama siku ya Jumamosi, Mei 16, huko Mpage. Idadi ni kubwa: raia wawili waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa, baadhi yao wakipelekwa hadi Mayotte.

Katika taarifa yake, ofisi ya mwendesha mashtaka inaahidi uchunguzi ambao itaufanya “bila upendeleo.” Serikali ilitoa rambirambi zake na kuwataka raia kuwa watulivu na kuepuka kusambaza uvumi au taarifa potofu.

Wapinzani, kwa upande wao, wametoa wito wa uchunguzi huru.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *