MAYELE NDANI YA KOMBE LA DUNIAMAYELE NDANI YA KOMBE LA DUNIA

MAYELE NDANI YA KOMBE LA DUNIA

Mshambuliaji wa Pyramids FC ya Misri, Fiston Mayele amejumuhishwa kwenye kikosi cha nyota 26 watakaounda timu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ‘The Leopards’ itakayoshiriki fainali za Kombe la Dunia 2026.

Mchezaji huyo wa zamani wa Yanga SC mwenye umri wa miaka 31 ambaye ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa CAF kwa wachezaji wa ndani ya Afrika 2025, anakuwa mchezaji pekee anayekipiga ndani ya Afrika kujumuhishwa kwenye kikosi hicho cha Kocha Sebastian Desabre.

DRC inarejea kwenye fainali za Kombe la Dunia baada ya miaka 72 tangu washiriki kwenye fainali za mwaka 1974 na mwaka huu wamepangwa kundi moja na Ureno, Colombia na Uzbekistan.

#FWC26 #FIFAWorldCup #WeAre26 #FIFAWorldCup2026NyumbaniAzamTV #MechiZote104LiveAzamTV

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *