Mgomo wa magari ya abiria watatiza shughuli nchini KenyaMgomo wa magari ya abiria watatiza shughuli nchini Kenya

Raia wa Kenya, hivi leo wamepata wakati mgumu kufika kwenye maeneo yao ya kazi kufuatia mgomo uliotangazwa na wamiliki wa magari ya abiria na bodaboda ulioanza hivi leo kushinikiza serikali kushusha bei ya mafuta.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tulizuru baadhi ya maeneo ya jiji la Nairobi katika barabara kuu ya Waiyaki ambapo sehemu kubwa ya wakazi wa eneo hilo walionekana wakitemebea kwa miguu, hapa, hakuna magari ya uchukuzi wa umma yalioonekana barabarani, ni bodaboda peke yake lakini pia bei yake imepanda maradufu.

Katikati mwa jiji hakukuwa magari ya uchukuzi wa umma, maofisa wa usalama walijitokeza kulinda usalama na kukabiliana na watu waliokuwa na nia ya kuandamana.

Katika mtaa wa Kangemi, Nje kidogo na jijini la Nairobi, Maandamano yamefanyika, hapa usafiri umetatizika.

Maofisa wa polisi wasiokuwa na sare rasimi wakimkamata mwandamaji jijjini Nairobi.
Maofisa wa polisi wasiokuwa na sare rasimi wakimkamata mwandamaji jijjini Nairobi. REUTERS – Thomas Mukoya

Hali kama hii ilishuhudiwa katika barabara nyengine za kuingia jijini Nairobi, wakaazi wamelazimika kutembea kwa miguu kufika kazini, kutokana na kutokuwepo kwa magari ya abiria.

Baadhi wametumia usafiri wa bodaboda chache zilizokuwepo ambazo hata hivyo zilikuwa zikilipisha bei ya juu zaidi.

Masomo pia yameathirika, wanafunzi wakitakiwa kusalia nyumbani. Mgomo huu wa wahudumu wa magari ya abiria umejiri ikiwa imepita siku chache tu tangu mamlaka nchini Kenya kuongeza bei ya mafuta kwa zaidi ya asilimia 20.

Wakenya waliokosa kupata usafiri wa umma wakitumia mbinu mbadala kufika walikokuwa wakienda.
Wakenya waliokosa kupata usafiri wa umma wakitumia mbinu mbadala kufika walikokuwa wakienda. REUTERS – Thomas Mukoya

Kwa sasa lita moja ya petroli jijjni Nairobi inauzwa kwa shilling 214.25 wakati diseli ikiiuzwa kwa shilling 242.92.

Kenya kama mataifa mengine ya Afrika, inategemea pakubwa mafuta kutoka katika nchi za Ghuba, usafirishaji wa bidhaa hiyo ukiathiriwa na mzozo kati ya Iran, Marekani na Israel ulioanza Februari 28.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *