Cape Verde: PAICV yarejea madarakani baada ya miaka kumi katika upinzaniCape Verde: PAICV yarejea madarakani baada ya miaka kumi katika upinzani

Chama cha mrengo wa kushoto, PAICV, kimeshinda uchaguzi, huku Waziri Mkuu Ulisses Correia e Silva, kiongozi wa Movement for Democracy (MpD), akikubali kushindwa. Mpito mpya wa kisiasa unakaribia Cape Verde, ingawa matokeo ya uchaguzi wa wabunge bado hayajakamilika.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi uligubikwa na ushiriki mdogo. Idadi ndogo ya wapiga kura, sawa na 50% pekee ya wapiga kura 415,000 waliojiandikisha ambao waliga kura. Kwa kuwa 98% ya kura zimehesabiwa, PAICV kwa sasa ina viti 35, MPD inabaki na viti 31, na UCID inashikilia nafasi yake ikiwa na viti 2. Matokeo ya viti vinne vilivyobaki vya diaspora bado hayajatolewa na Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (CNE). Tume ya Uchaguzi ilibainisha kwamba matokeo ya mwisho ya uchaguzi huu wa wabunge yatatangazwa Mei 25.

Akiwa mkuu wa nchi tangu mwaka 2016, na kuchaguliwa tena mwaka wa 2021, Ulisses Correia e Silva hakusubiri kutangazwa kwa matokeo ya mwisho ili kukiri kushindwa kwake na kwa chama chake. “Nilimpigia simu kiongozi wa chama ch PAICV kumpongeza kwa matokeo hayo na kumtakia kila la heri katika utawala wake, ambao unaendelea kuhakikisha utawala bora nchini Cape Verde,” Waziri Mkuu anayemaliza muda wake alisema katika makao makuu ya Movement for Democracy. “Sasa natoa wito kwa rais wa PAICV kuiangalia Cape Verde kwa jicho la heri, mapenzi na huruma. “

Kiongozi wa chama cha PAICV, Francisco Carvalho, anatarajiwa kuwa kiongozi mpya wa Cape Verde. Kwa mpango wake unaozingatia haki ya kijamii, hasa upatikanaji wa huduma za afya, elimu ya juu, na huduma bora za usafiri, mwanasiasa huyo, meya wa mji mkuu Praia, alifanikiwa kuwashawishi wapiga kura: “Mradi wa ‘Cape Verde for All’ ulikuwa bora zaidi, kwa sababu ni mradi uliojengwa kutokana na mahitaji ya Wacape Verde na unaendana na mradi tunaotaka kujenga.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *