Marekani na Nigeria zatekeleza mashambulizi mapya dhidi ya kundi la Islamic StateMarekani na Nigeria zatekeleza mashambulizi mapya dhidi ya kundi la Islamic State

Nigeria na Marekani zimefanya operesheni mpya dhidi ya kundi la Islamic State kaskazini mashariki mwa Nigeria, ambapo uasi wa wanajihadi umekuwa ukiendelea kwa miaka kumi na saba.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatatu, Mei 18, Africom – Kamandi ya Marekani barani Afrika – ilithibitisha kwamba ilifanya mashambulizi mapya ya anga siku ya Jumapili, Mei 17, saa 24 baada ya kumuua kiongozi mkuu wa ISIS nchini humo. Ushirikiano wa kijeshi kati ya Washington na Abuja umekuwa ukiimarika kwa miezi kadhaa katika mapambano dhidi ya wanajihadi.

“Hizi zilikuwa operesheni sahihi, zilizopangwa kwa uangalifu na ngumu sana,” ilisema mamlaka ya Nigeria, ambao ilibainisha kwamba hakuna mwanajeshi kutoka Marekani aliyeshiriki katika operesheni ya kikosi cha nchi kavu. “Wamarekani walitoa taarifa za kijasusi,” aliongeza msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Nigeria.

Mashambulizi hayo yalijikita karibu na Metele na Dogon Chukwu, kaskazini mwa Jimbo la Borno, kwenye mpaka na Niger na Chad. Karibu wapiganaji ishirini wa kundi la Islamic State (ISIS) waliuawa, akiwemo kiongozi mkuu wa ISIS huko Afrika Magharibi, Abu-Bilal al-Minuki, na baadhi ya maafisa wake.

Picha zilizotolewa na Africom zinaonyesha mashambulizi ya anga kwenye kundi la watu waliokuwa kwenye pikipiki na majengo. Hata hivyo, kulingana na Gazeti la New York Times, kikosi cha makomandoo cha wanajeshi wa Marekani kilishiriki katika shambulio kwenye makazi ya al-Minuki.

Mnamo mwezi Desemba mwaka uliyopita, jeshi la Marekani, kwa ushirikiano na mamlaka ya Nigeria, tayari lilifanya mashambulizi ya anga siku ya Krismasi dhidi ya wapiganaji wa ISIS katika Jimbo la Sokoto, rasmi ili kuwaunga mkono Wakristo nchini Nigeria.

Kwa watafiti, ushiriki huu wa Marekani katika miezi ya hivi karibuni unaonyesha nia inayoongezeka kutoka Washington.

Tawi la kundi la Islamic State katika Afrika Magharibi sasa linachukuliwa kuwa ndilo lenye shughuli nyingi na uwezo zaidi wa kundi la wanajihadi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *