RDC: Wakaazi wa Bukavu wanachukua hatua zipi kujikinga na msambao wa EbolaRDC: Wakaazi wa Bukavu wanachukua hatua zipi kujikinga na msambao wa Ebola

Mashariki mwa DRC, maambukizi hatari ya virusi vya Ebola, yameendelea kuzua hofu ya kusambaa zaidi, wakati huu idara za afya nchini humo zikisema watu zaidi ya 100 wamethibitishwa kufa kutokana na ugonjwa huo. Lakini je wakazi wa Bukavu wanachukua tahadhari gani huko Kivu Kusini?

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika vitongoji kadhaa vya Bukavu, wakaazi sasa wanahimizwa na kuhimizana kuzingatia sheria za usafi. Sokoni na dukani, watu wanazingatia usafi wa mikono.

Louise Cubaka ni Mkaazi wa Bukavu.

“Kwangu kwa nyumba nina ndoo, watoto na wageni wakifika lazima wanawe mikono.” Alisema Louise Cubaka ni Mkaazi wa Bukavu.

Lakini Alain Zaluke, mkaazi mwingine wa Bukavu, anaeleza kwamba changamoto kubwa ni upatikanaji wa maji kwa ajili ya usafi.

“Maji Bukavu ni changamoto kwa hivyo ile ambayo ipo kwa nyumba lazima tuichunge sana.” Alisema Alain Zaluke.

Mamlaka ya afya kwa ushirikiano na mashirika kadhaa ya kibinadamu, imeimarisha hatua za ufuatiliaji katika mipaka ya kuingia Bukavu.

Akiwa mkazi wa kivu kusini, Justin Murhabazi amewaonya wakazi wenzake kuzingatia mikakati yakujikinga licha yakuwa Ebola iliwahi kuripotiwa Congo tangu awali.

Katika tangazo la hivi karibuni, gavana wa Kivu kusini chini ya uthibiti wa AFC/M23 Patrick Busu bwa Ngwi amewataka wakazi kuzingatia mbinu za kupambana na  Ebola ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara, kuepuka kuwasiliana na watu wanaoonyesha dalili zinazoshukiwa kuwa za Ebola.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *