Wizara Ulinzi yaja na maeneo manane bajeti ikipitaWizara Ulinzi yaja na maeneo manane bajeti ikipita

Dodoma. Bunge limepitisha bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ya Sh4.3 trilioni kwa mwaka wa fedha 2026/27 ambayo imepangiwa maeneo manane ya utekelezaji.

Kati ya fedha hizo, Sh426.5 bilioni zimepangiwa matumizi ya maendeleo katika baadhi ya malengo ikiwemo kuimarisha jeshi kwa zana na vifaa vya kisasa, kiteknolojia, mawasiliano na rasilimali watu.

Akiwasilisha bajeti hiyo leo, Jumanne Mei 19, 2026, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Rhimo Nyansaho ametaja baadhi ya maeneo yaliyoangaziwa ni kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi kwa wanajeshi, vifaa na zana, mazoezi, mafunzo, masilahi, huduma za afya na makazi.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, tutaendelea kuimarisha uwezo wa Jeshi la Kujenga Taifa, kuliimarisha Jeshi la Akiba, kulinda miradi ya kimkakati na kuimarisha mashirika na taasisi za utafiti wa masuala ya kijeshi na kuanzisha viwanda katika sekta ya ulinzi (Defence industries),” amesema Waziri Dk Nyansaho.

Waziri amesema wataimarisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki na kati na masuala ya ulinzi, lakini wanalenga kushirikiana na mamlaka za kiraia katika kukabiliana na majanga inapohitajika.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  Dk Rhimo Nyansaho (wa tatu kushoto)akipongezwa na makatibu wakuu wastaafu pamoja na viongozi wastaafu wa wizara yake mara baada ya kupitishwa kwa bajeti ya wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha wa 2026/2027 Bungeni jijini Dodoma. Kulia ni  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali, Jacob John Mkunda. Picha na Said Khamis

Ametaja malengo katika bajeti hiyo ni kuimarisha uIinzi na amani, kuwa jeshi imara Ienye wataaIamu, zana, na vifaa vya kisasa katika kujenga uwezo, tafiti na uhawiIishaji wa teknoIojia kwa matumizi ya kijeshi na kiraia, kuimarisha Jeshi Ia Akiba na kusaidia mamIaka za kiraia na majanga iIi kuwapatia waathirika msaada wa kibinadamu.

Ulinzi mipakani

Waziri amesema katika mwaka wa fedha 2025/26, hali ya mipaka ya Tanzania yenye urefu wa kilomita 5,923.41, inayohusisha eneo la nchi kavu, anga na eneo la maji, imekuwa ni salama licha ya changamoto ndogondogo.

Nchi zinazopakana na Tanzania ni Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Kenya, Malawi, Msumbiji, Rwanda, Uganda, Zambia na mipaka ya Bahari ya Hindi inayojumuisha visiwa vya Comoro na Shelisheli.

Katika maeneo yote amesema kuna usalama isipokuwa mpaka wa Msumbiji wenye urefu wa kilomita 922.76, unakabiliwa na changamoto ya uwepo wa kikundi cha kigaidi cha Ansar Al – Sunna Wal Jamaah (ASWJ), Islamic State Mozambique Province huku mpaka wa Uganda wafugaji wanaingiza mifugo yao katika Wilaya ya Misenyi bila utaratibu.

Akihitimisha hoja yake, ametaja kuwa malengo ya Dira ya Taifa ya 2050 hayawezi kufikiwa ikiwa Taifa linakosa amani na ulinzi madhubuti kwa mipaka na wananchi wake hivyo akaomba amani iwe ni kipaumbele.

Maoni ya kamati

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), Najma Giga amesema ili kuimarisha vikosi vya ulinzi, upatikanaji wa fedha za maendeleo kwa wakati na kwa kiwango stahiki, ni muhimu uendelee kupewa kipaumbele ili malengo yafikiwe.

Giga pia amezungumzia umuhimu wa kuwepo kwa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili kuwajengea uzalendo, ukakamavu, umoja wa kitaifa, na stadi za maisha na kazi vijana.

Ameomba fursa za mafunzo hayo ziongezwe kwa vijana akisisitiza ulipaji wa fidia kwa maeneo yaliyofanyiwa uthamini kwa lengo la kutwaliwa kwa shughuli za ulinzi ili wananchi wanaohamishwa wawezeshwe au kuendeleza shughuli za kiuchumi na kijamii katika maeneo mengine.

“Upatikanaji wa fedha za kulipa fidia kwa wananchi wanaohamishwa kupisha shughuli za kiulinzi na malipo ya fidia stahiki kwa wakati unapunguza adha kwa wananchi kuendelea kusubiri fidia, au kuwepo katika maeneo hayo wasiyopaswa kuyaendeleza,” amesema Giga.

Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu ameomba Serikali kuendelea kuwatunza na kuwathamini askari waliopigana vita ya Kagera kwani baadhi yao kwa sasa maisha yao ni magumu na akasifia kazi inayofanywa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika zao

New Content Item (1)

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  Dk Rhimo Nyansaho (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali, Jacob John Mkunda mara baada ya kuwasili mkatika viwanja vya Bunge jijini Dodoma ,Leo Wizara ya Ulinzi inatarajiwa kuwasilisha Bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2026/2027

Hata hivyo, ameomba jeshi kulinda heshima yake kwa kujitenga kabisa na siasa ili wasije kuingia kwenye lawama.

Mbunge wa Viti Maalum, Zainabu Abdallah Issa ameiomba Serikali kuongeza uwezo wa kibajeti kwa jeshi ili vijana wengi wanaomaliza kidato cha sita wajiunge na mafunzo kwa wingi kuliko ilivyo sasa, ambapo uwezo wa kuwachukua ni 60,000 wakati wanaomaliza ni zaidi ya 100,000.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *