
Wabunge wa Bunge la Ulaya na nchi wanachama wa EU wamefikia makubaliano ya muda ya kutekeleza makubaliano ya biashara yaliyohitimishwa msimu uliopita wa joto na Marekani, ofisi ya rais wa Kupro inayosikiliwa urais wa kupokezana wa EU imetangaza mapema Jumatano asubuhi. “Baraza na Bunge zimefikia makubaliano kuhusu utekelezaji wa vifungu vya ushuru wa Azimio la Pamoja la EU-Marekani lililopitishwa mnamo Agosti 21, 2025.”
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Rais wa Marekani Donald Trump anatishia EU kwa ushuru mpya ikiwa makubaliano hayo hayataidhinishwa ifikapo Julai 4.
Haya ni makubaliano yaliyofikiwa dakika za mwisho na chini ya tishio la ushuru wa Marekani. Umoja wa Ulaya umefikia makubaliano ya muda leo Jumatano usiku kuhusu kuondolewa kwa ushuru wa bidhaa za Marekani, ili kuzingatia makubaliano ya biashara yaliyohitimishwa na Marekani mwaka jana na kuepuka tishio la Rais wa Marekani Donald Trump la kutoza ushuru wa juu zaidi.
Chini ya makubaliano yaliyofikiwa mwezi Julai mwaka uliyopita, EU ilikubali kuondoa ushuru wa bidhaa za viwandani za Marekani na kutoa ufikiaji wa upendeleo kwa bidhaa za kilimo na uvuvi za Marekani. Kwa kubadilishana, Marekani ilipaswa kutoza ushuru wa 15% kwa bidhaa nyingi za EU. Makubaliano yaliyofikiwa chini ya shinikizo kutoka kwa Rais wa Tume Ursula von der Leyen huko Turnberry, Scotland, katika hoteli ya gofu ya Donald Trump, yalikosolewa vikali, haswa kutoka Ufaransa, Ujerumani, na wabunge wa Bunge la Ulaya. Rais wa Tume alishutumiwa kwa kuchukuwa uamuzi wa upande mmoja.
Mchakato mgumu
Bunge la Ulaya kisha likapeleka suala hilo kwa Mahakama ya Haki ya EU ili kuthibitisha usahihi wa maandishi hayo na mikataba hiyo. Hata hivyo, ombi la Bunge la kusitisha makubaliano hayo, likisubiri maoni ya Mahakama, halikuwa la lazima kwa Tume—ambayo ina uwezo wa kipekee katika masuala ya biashara ya nje—kwa hivyo mnamo mwezi Februari 2026, Ursula von der Leyen alitangaza matumizi ya muda ya vifungu vya maandishi hayo, na kusababisha tena hasira kutoka Ufaransa tena.
Bunge la Ulaya liliidhinisha kwa masharti makubaliano ya biashara yaliyofikiwa mwezi Machi, lakini taratibu za ndani za kambi hiyo zinahitaji mazungumzo na nchi wanachama kabla ya kutekelezwa rasmi.
Mwanzoni mwa mwezi Mei, rais wa Marekani alirejelea mashambulizi yake. “Kwa kuzingatia kwamba Umoja wa Ulaya hauzingatii makubaliano yetu ya biashara yaliyokamilishwa kikamilifu, nitaongeza ushuru kwa magari na malori yanayoingia Marekani wiki ijayo,” aliandika katika chapisho kwenye mtandao wake wa kijamii, Truth Social. Donald Trump alitangaza kuwa alikuwa akiupa Umoja wa Ulaya hadi Julai 4 kutekeleza makubaliano ya biashara, baada yaysimu na Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen.
Karibu miezi kumi baada ya mkutano wa mwezi Julai 2025, Bunge la Ulaya na Baraza la EU, chombo kinachowakilisha serikali za kambi hiyo, wamekubaliana kuhusu maandishi ya kisheria, na kufungua njia ya kuanza kutumika kwa upunguzaji wa ushuru wa EU.
“Ninajivunia kutangaza kwamba Ulaya imeepuka ongezeko baya la mvutano wa kibiashara na imelinda biashara za Ulaya, uwekezaji, na mamilioni ya ajira pande zote mbili za Atlantiki,” Zeljana Zovko, mjadili mkuu wa Chama cha EPP kwa makubaliano haya, amesema kwenye mtandao wa kijamii wa X, kulingana nashirika la habari la REUTERS.
Kura ya mwisho ya kuidhinisha katika Bunge la Ulaya imepangwa kufanyika katikati ya mwezi Juni.
