Tehran imesema leo Jumatano kwamba nchi za Ghuba zina “jukumu la kisheria na kimaadili” la kusitisha mashambulizi ya Marekani yaliyoanzishwa dhidi ya Iran kutoka maeneo yao, na kuhalalisha mashambulizi zaidi ya Iran dhidi ya nchi jirani ambako kinapatikana kambi za Marekani.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran “imebainisha jukumu la kisheria na kimaadili la nchi zote katika eneo hilo (…) kuzuia jeshi la Marekani na Israel kutumia eneo au vifaa vyao kupanga, kutekeleza, au kuunga mkono vitendo vya uadui dhidi ya Iran,” kulingana na taarifa.

Wizara hiyo imeonya kwamba Iran “haitasita kutumia haki yake ya asili ya kujilinda,” hasa ikilenga kambi na vifaa vya usafirishaji vinavyotumika kwa operesheni dhidi ya Iran.

Wakati huo huo Iran imetangaza leo Jumatano kwamba imelenga kambi za Marekani katika Ghuba ili kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya Washington dhidi ya malengo ya Iran kando ya Mlango-Bahari wa Hormuz, katika mvutano mpya baada ya helikopta ya Marekani kuharibiwa, kitendo kilichohusishwa na Tehran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *