Mali: Raia wanaendelea kuuawa na wanajihadi wa JNIM Tonka, karibu na TimbuktuMali: Raia wanaendelea kuuawa na wanajihadi wa JNIM Tonka, karibu na Timbuktu

Abdoul Salam Maïga, mwalimu wa Quran katika madrasa huko Tonka, amepigwa risasi hadharani na wanajihadi wa JNIM siku ya Alhamisi, Mei 21. Mamo mwezi Novemba mwaka uliyopita, mji huuulioko katikati ya nchi ulikuwa tayari ukiomboleza kuuawa hadharani kwa Mariam Cissé, mwanamke ambaye alikuwa mtayarishaji wa video fupi na maudhui katika mtandao wa kijamii wa TikTok, ambaye alionyesha uungaji mkono wake kwa jeshi la Mali.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Abdoul Salam Maïga, mwalimu wa Quran katika madrasa huko Tonka, alikuwa akizungumza kwa amani na marafiki katika kundi la majadiliano ya kitamaduni) karibu na soko wakati wapiganaji wa kijihadi wa JNIM waliokuwa na silaha walipotokea ghafla na kumwamuru awafuate. Kulingana na viongozi kadhaa wa eneo hilo waliowasiliana na RFI, walirudi muda mfupi baadaye. Abdoul Salam Maïga alifungwa macho. Kisha akauawa hadharani kwa kupigwa risasi.

Kulingana na baadhi, mauaji yake yanaweza kuhusishwa na tofauti za kidini. “Labda alikataa kuwafanyia kazi,” chanzo kimoja kimebainisha. Lakini kwa wengi wa waliohojiwa, ni uhusiano wake wa karibu na jeshi la Mali uliosababisha kundi hili la JNIM kutekeleza mauaji ya mwalimu huyo wa Quran.

Mnamo mwezi Novemba mwaka uliyopita, Tonka na Mali nzima walikuwa tayari wakiomboleza kuuawa hadharani kwa Mariam Cissé, mwanamke ambaye alikuwa mtayarishaji wa video fupi na maudhui katika mtandao wa kijamii wa TikTok, ambaye aliunga mkono hadharani jeshi la Mali.

Kisha, mwishoni mwa mwezi Machi, Amadou Baby, kiongozi wa shirika la vijana katika wilaya ya Tonka, alipigwa risasi mtaani. Chama chake kilishukiwa na wanajihadi kutoa taarifa za kijasusi kwa vikosi vya jeshi la Mali, ingawa baadhi ya vyanzo vilivyowasiliana na RFI vilibainisha kwamba katika mji wa Tonka hakukuwa na kambi ya kijeshi.

“Huko Tonka, Diré, Goundam, na Timbuktu, watu wamesikitishwa na mauaji haya yote,” mkazi mmoja wa eneo hilo amesema. “mauaji haya yamewakasirisha wakazi wa eneo lote.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *