Serikali imesema mpango wa ujenzi wa magati 11 mapya katika Bandari ya Dar es Salaam unatarajiwa kuongeza uwezo wa bandari hiyo kuhudumia shehena kubwa zaidi za mizigo na kuimarisha nafasi ya Tanzania kama kitovu cha biashara na usafirishaji katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini.
Akizungumza baada ya ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) bandarini hapo, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema uwekezaji huo unaenda sambamba na maboresho ya miundombinu ya reli na huduma za uchukuzi kwa lengo la kuongeza ushindani wa kiuchumi na kuvutia biashara ya usafirishaji kutoka nchi jirani.
Naye Mwenyekiti wa kamati hiyo, Masanja Kadogosa amesema maboresho hayo yataongeza mchango wa sekta binafsi katika uchumi, kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo na kuimarisha ushindani wa Bandari ya Dar es Salaam dhidi ya bandari nyingine za kikanda ikiwemo Mombasa na Durban.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)
