Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polis (ACP)Zauda Mohamed, amewaomba wamiliki na madereva wa vyombo vya moto vinavyotoa huduma za usafirishaji maarufu kama “daladala” mkoani humo kukaa pamoja na mamlaka husika, ikiwemo Jeshi la Polisi, ili kutafuta suluhisho la mgomo huo na kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.
Hatua hiyo imekuja baada ya watoa huduma hao Jijini Arusha mapema leo kugoma kutoa huduma, wakidai kutokupewa taarifa za faini wanazotozwa na LATRA, mamlaka inayosimamia udhibiti wa usafiri wa ardhini.
Kwa upande wake, kiongozi kutoka LATRA amewaomba viongozi wa madereva hao kukaa pamoja na mamlaka hiyo ili kujadili changamoto zao walizonazo ili kwa pamoja kutafuta suluhisho la kudumu kwa changamoto hizo.
(Feed generated with FetchRSS)
