“VIJANA CHANGAMKIENI FURSA ZILIZOFUNGULIWA NA SERIKALI”- MWASELELA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema Rais Samia Suluhu Hassan ameweka matumaini makubwa kwa vijana wa Kitanzania katika kuhakikisha Tanzania inapiga hatua kimaendeleo.
Kimesema uwapo wa vijana wenye maadili na wachapakazi unatoa fursa kubwa kwa Tanzania kupiga hatua kubwa kwenye maendeleo katika njanja zote ikiwemo kiuchumi na kijamii.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mkoa wa Mbeya, Ndele Mwaselela akizungumza na vijana kwenye kongamano la elimu lililohusisha wanafunzi wa Kiislamu wa Elimu ya Juu na Kati (TAMSYA).
“Serikali imeunda wizara kwa ajili ya vijana hivyo, tutumie fursa hii kushiriki kwenye shughuli za maendeleo na ujenzi wa Taifa kwani, Rais Samia ameweka mazingira bora na wezeshi kwa vijana.’
Amesisitiza umuhimu wa vijana kuendelea kuwa wazalendo kwa Tanzania ikiwemo kufanya kazi kwa bidii na kuwa mabalozi wa amani.
(Feed generated with FetchRSS)
