Rezaei: Iran itajiondoa katika mkataba wa kuzuia silaha za nyuklia iwapo itashambuliwa tenaRezaei: Iran itajiondoa katika mkataba wa kuzuia silaha za nyuklia iwapo itashambuliwa tena

Iran imetoa onyo kali kwa Marekani, ikisema kuwa itajiondoa kwenye Mkataba wa Kuzuia Usambazaji wa Silaha za Nyuklia (NPT), ikiwa Marekani itaanzisha tena mashambulizi dhidi ya yake.

Akizungumza katika hafla ya kuwakumbuka mashahidi wa vita vya hivi karibuni vya kichokozi vilivyoanzishwa na Marekani na utawala wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Meja Jenerali Mohsen Rezaei, mshauri mwandamizi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, amesisitiza kuwa mpango wa nishati ya nyuklia wa Tehran ni wa amani na uko chini ya uangalizi wa mara kwa mara wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).

Rezaei, ambaye ni kamanda wa zamani wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), ameongeza kuwa chini ya mwongozo wa Kiongozi Muadhamu, timu ya mazungumzo ya Iran imeweka msimamo thabiti kwa Marekani kuwa haitarudi nyuma hata kidogo katika haki zake za kimsingi za nyuklia.

Ameendelea kwa kuionya Marekani kuwa, “Mkiingia katika Ghuba ya Uajemi, kwanza kabisa, tutatoa jibu kali, lenye maumivu na ambalo halijawahi kushuhudiwa, na tutavunja mzingior wa baharini majini.” Kisha amesema: “Lakini muhimu zaidi, tunaweza kujiondoa kwenye NPT. Je, mnafahamu nini kitawakumba iwapo tutachukua hatua hiyo? Hivyo basi… msijitumbukize kwenye kifo.”

Akigusia hali ya sasa ya taharuki katika eneo hili, Jenerali Rezaei amesisitiza kuwa Iran iko tayari kabisa kijeshi kukabiliana na uchokozi wowote dhidi yake. Amesema kuwa Jeshi la Wanamaji la IRGC ndilo linalosimamia Lango la Hormuz ili kuzuia hujuma na ukosefu wa usalama katika Ghuba ya Uajemi, kwa kusajili na kutambua vyombo vya baharini vinavyopita katika njia hiyo muhimu ya biashara huru.

Ametoa onyo kwa Rais wa Marekani Donald Trump na utawala wake kwamba vita havitaishia katika Lango la Hormuz pekee, bali vitaenea hadi Bahari ya Shamu, mlango wa Bab el-Mandab, na Bahari ya Hindi iwapo wataingia katika Ghuba ya Uajemi.

Iran ilifunga njia ya bahari ya Hormuz kwa maadui zake na washirika wao kufuatia uchokozi wa Marekani na Israel. Mamlaka ya Iran ilianza kutekeleza udhibiti mkali zaidi mwezi uliopita baada ya Trump kutangaza vizuizi vinavyolenga meli na bandari za Iran.

Iran inasema hatua za Marekani ni ukiukaji wa makubaliano ya usitishaji vita yaliyosimamiwa na Pakistan, ambayo yalianza kutekelezwa tarehe 8 Aprili na baadaye kuongezwa muda wake na Washington kwa upande mmoja. Licha ya vizuizi hivyo vya Marekani, shughuli za usafirishaji wa mafuta ghafi yanayohusishwa na Iran zinaonekana kuendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *