Baqaei: Marekani imefanya uhalifu wa kivita kwa kujaribu nguvu ya kombora lilitumika kwa mara ya kwanza kuua watu Lamerd, IranBaqaei: Marekani imefanya uhalifu wa kivita kwa kujaribu nguvu ya kombora lilitumika kwa mara ya kwanza kuua watu Lamerd, Iran

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: “Marekani ilitumia kwa mara ya kwanza kombora la PrMS katika shambulio lake kwenye eneo la makazi ya raia na uwanja wa michezo wa Lamerd katika Mkoa wa Fars kusini mwa Iran, kwa lengo la kujaribu nguvu za uharibifu za silaha hiyo.”

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmail Baqaei ameandika katika ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii kwamba: “Wakati wa mkutano wangu na Musa Mousavi, mwakilishi wa jimbo la Mehr na Lamerd katika Bunge la Iran, nimearifiwa kuhusu baadhi ya maelezo ya uhalifu wa kutisha wa Marekani katika shambulio la kombora kwenye ukumbi wa michezo katika mji wa Lamerd, Mkoa wa Fars.”

Baqaei amesema: Jioni ya Jumamosi, Februari 28, 2026; siku hiyo hiyo ambayo Marekani iliua shahidi wanafunzi wa Shule ya Msingi ya “Shajare Tayyiba” huko Minab, mkoa wa Hormozgan kwa makombora matatu ya Tomahawk, eneo la makazi ya raia katika mji wa Lamerd, ikiwa ni pamoja na ukumbi wa michezo, pia lililengwa kwa makombora manne ya PrMS. Kufuatia mlipuko wa makombora hayo, watu 24, ikiwa ni pamoja na msichana wa miaka miwili, wachezaji kadhaa wa mpira wa wavu vijana, na wanaume na wanawake kadhaa wasio na hatia, waliuawa shahidi. Zaidi ya watu 130 pia walijeruhiwa, idadi kubwa miongoni mwao wakiwa na ulemavu wa kudumu.

“Kabla ya kulenga shabaha, makombora hayo yalilipuka angani na kuwa zaidi ya vipande 180,000 vilivyojumuisha chembechembe za tungsten; vipande vilivyotawanyika pande zote kwa kasi na nguvu kubwa,” ameongeza Esmail Baqaei.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: “Shambulio hilo halikufanyika kimakosa; sasa hakuna shaka kwamba jeshi la Marekani lilitumia aina hii ya makombora kwa mara ya kwanza katika eneo la makazi ya raia na ukumbi wa michezo katika mji wa Lamerd kwa lengo la kujaribu nguvu ya uharibifu ya silaha hizo.” Ameongeza kuwa Kitendo hiki ni uhalifu wa kivita wa kutisha na usiosameheka, na makamanda na wahusika wake lazima washtakiwe katika mahakama husika.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *