Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo nchini (STPU), kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Ufugaji, kimemka…Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo nchini (STPU), kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Ufugaji, kimemka…

Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo nchini (STPU), kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Ufugaji, kimemkamata mtuhumiwa mmoja aliyekuwa akijaribu kutorosha mbuzi na kondoo 320 kwenda nchi jirani kinyume cha sheria.

Kamanda wa kikosi hicho, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Simon Pasua, amesema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kumefanyika wakati wa doria ya pamoja Wilaya ya Longido, mkoani Arusha, Mei 25, 2026 na kuongeza kuwa, mtuhumiwa alikuwa na wenzake ambao walifanikiwa kutoroka.

Jeshi la Polisi limewataka wafugaji na wafanyabiashara kufuata sheria za usafirishaji wa mifugo, huku likisisitiza ushirikiano wa wananchi katika kutoa taarifa za uhalifu.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *