Wafanyabiashara watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni Jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na mashtaka tisa…Wafanyabiashara watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni Jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na mashtaka tisa…

Wafanyabiashara watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni Jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na mashtaka tisa yakihusisha kuingiza magari yenye namba za usajili za Afrika Kusini na kuyatumia nchini bila kufuata taratibu za kiforodha.

Kutokana na udanganyifu huo wafanyabiashara hao wanadaiwa kuisababishia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hasara ya zaidi ya Sh100 milioni.

Washtakiwa hao ni George Kaiza (35), Hosiana Sanga (31) na Hamu Sanga (26) wote wakidaiwa kutoa matamko ya uongo kwa maofisa wa forodha wa TRA katika mipaka ya Tanzania na kuingiza magari yenye usajili wa namba za kigeni na kuyatumia bila kufuata taratibu za kiforodha.

Washtakiwa wote wamefikishwa mahakamani hapo Mei 26,2026 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhani Rugemalila na kusomewa mashitaka yao na Wakili wa Serikali Godfrey Nugu akisaidizana na Rozalia Rutagwerela.

Akisoma hati ya mashitaka, Wakili Nugu alidai wote watatu wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye jumla ya mashitaka tisa, huku kesi namba 11588 ya mwaka 2026 yenye mashitaka saba inamkabili Kaiza pekee yake.

Magari hayo ni aina ya Ford na Toyota Fortuner ambako baada ya kusomwa mashtaka hayo, hakimu Rugemalila alimuonya Kaiza kuwa hakutakiwa kujibu chochote kwa sababu Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi ambako ilidaiwa kuwa upelelezi bado unaendelea na kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 9, 2026 kwa ajili ya kutajwa. Watuhumiwa wote wamerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *