#HABARI: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe, amesisitiza kuwa Serikali haitomuongezea muda Mkandarasi M/s China Civil Engineering Construction Corporation wa kukamilisha mradi wa barabara na mitaro katika Manispaa ya Kahama.
Akizungumza wakati wa utiaji saini wa mkataba huo wa mradi wa TACTIC uliofanyika eneo la Phantom, Prof. Shemdoe amemtaka mkandarasi huyo kukamilisha kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa kwa sababu ubovu wa miundombinu hiyo umekuwa kero ya muda mrefu kwa wananchi.
Mradi huo mkubwa unagharimu zaidi ya shilingi bilioni 25.5 (bila VAT), fedha zilizoridhiwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kama sehemu ya kutekeleza ahadi zake za kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Prof. Shemdoe amemuelekeza mtaalamu mshauri, TARURA, na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama kushirikiana kikamilifu kusimamia mradi huo ili ukamilike kwa ubora na kuleta thamani halisi ya fedha zilizowekezwa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, amebainisha kuwa mradi huo wa TACTIC utatekelezwa kwa awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza inahusisha ujenzi wa barabara za katikati ya mji zenye urefu wa kilomita 12.3 na mifereji ya maji ya mvua.
Mratibu wa miradi hiyo kutoka TARURA, Mhandisi Humphrey Kanyenye, amefafanua kuwa ujenzi huo utachukua muda wa miezi minane kuanzia Juni 1, 2026, hadi Januari 31, 2027.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania
(Feed generated with FetchRSS)
