Liverpool imefanya uamuzi wa ghafla wa kuachana na meneja wake Arne Slot ikiwa ni matokeo ya timu hiyo kutofanya vizuri katika msimu wa 2025/2026.

Mwandishi nguli wa habari za usajili, Fabrizio Romano ameripoti kwamba uongozi wa Liverpool umeamua kubadilisha uamuzi wake kuhusu Slot na sasa ataonyeshwa mlango wa kutokea.

Awali ilionekana kwamba kibarua cha Slot kipo salama licha ya kushindwa kutetea taji la Ligi Kuu England (EPL), msimu wa 2025/2026 lakini klabu hiyo imemuonyesha mlango wa kutokea.

Liverpool haijaishia tu kushindwa kutetea taji lake la EPL bali pia imeambulia patupu katika mashindano mengine na sasa inaonekana inataka kujipanga upya.

Inaonekana kama presha za mashabiki zimechangia kwa kiasi kikubwa uongozi wa klabu hiyo kumpiga chini Slot.

Inaripotiwa kwamba Meneja wa Bournemouth, Andoni Iraola ndiye anapewa nafasi kubwa ya kuwa mrithi wa Slot ndani ya Liverpool.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *