Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Ilala, Joyce Maketa, amesema malezi bora yanayozingatia maadili na imani ni msingi muhimu wa kumjenga mtoto na kumpa uwezo wa kuishi kwa kujiamini ndani ya jamii. Amesema watoto wanaolelewa katika mazingira yenye upendo na maelekezo sahihi hukua wakiwa na uthubutu na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi hata katika maisha yao ya baadaye.
Maketa ameeleza kuwa matumizi ya lugha kali na maneno ya kumkatisha tamaa mtoto yanaharibu saikolojia yake na kupunguza kiwango cha kujiamini, hali inayoweza kumzuia kufikia uwezo wake kamili anapokua. Amesisitiza kuwa wazazi wanapaswa kutumia njia za mazungumzo yenye staha na maelekezo chanya pale mtoto anapokosea.
✍ Ibrahim Kilumbo
Mhariri | John Mbalamwezi
@goodluckpaul_mc
@balqis_njuki
#AzamTVupdates
(Feed generated with FetchRSS)