Chama Cha Mapinduzi CCM kimesisitiza kuwa kimedhamiria kufanya Mageuzi makubwa katika sekta zote nchini ili kupeleka maendeleo Kwa wananchi kwakuwa Chama hicho kina nia ya dhati ya kuwainua kiuchumi Watanzania.
Ujumbe huo umetolewa Leo Jumapili Mei 31/2026 na Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na mafunzo CCM Kenani Kihongosi katika Mkutano wa hadhara Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro wakati akisikiliza na kutatua kero za wakazi wa Wilaya hiyo
Kihongosi amesema Chama Cha Mapinduzi CCM ndiyo Chama pekee chenye uwezo wa kuwapelekea maendeleo wananchi hivyo amewasihi wananchi kuwakataa wanasiasa wanaosema hakuna kilichofanyika wakati maendeleo yanaonekana.
Hayo yanajiri ikiwa ni sehemu ya ziara yake Mkoani Kilimanjaro yenye lengo la kufuatilia uhai wa Chama Cha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo ameonesha kuridhishwa na yaliyofanyika.
(Feed generated with FetchRSS)