#HABARI: Watu saba wameuawa na wengine 11 kujeruhiwa baada ya ndege isiyo na rubani kushambulia basi la abiria lililokuwa likisafiri kupitia sehemu inayodhibitiwa na Urusi, nchini Ukraine.
Kiongozi aliyeteuliwa na Urusi wa eneo la mashariki mwa Donetsk nchini Ukraine, Denis Pushilin, amesema basi hilo limeshambuliwa mapema leo Juni 03, 2026 lilipokuwa likisafiri kati ya Moscow na Simferopol, katika eneo la Crimea inayokaliwa na Urusi.
Urusi imedondosha ndege zisizokuwa na rubani zaidi ya 350 usiku kucha, kulingana na maafisa wa Urusi.
Hii inafanyika siku moja baada ya shambulio kubwa la Urusi katika miji kote Ukraine na kuua watu wasiopungua 22, wakiwemo wanawake na watoto kadhaa.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)