
Maeneo manne muhimu katika kambi ya anga na kituo cha amri na udhibiti cha jeshi la mauaji ya watoto la Marekani huko Al-Azraq, Jordan yameshambuliwa usiku wa kuamkia leo kwa makombora ya Jeshi la Walinzi wa Jamhuri ya Kiislamu (IRGC).
Taarifa iliyotolewa na Idara ya Uhusiano wa Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu imesema: Baada ya operesheni iliyofanikiwa ya Jeshi la Wanamaji la IRGC ya kupiga malengo 21 katika kambi za anga na majini za Marekani katika eneo la Magharibi mwa Asia na kuangusha ndege isiyo na rubani aina ya MQ9 katika anga ya mji wa Jam, na kwa kutilia maanani mwendelezo wa matendo maovu ya adui na kukamilisha operesheni ya kulipiza kisasi, vikosi vya Jeshi la Uislamu na wapiganaji shupavu wa Kikosi cha Anga cha IRGC wamepiga na kuharibu malengo 4 muhimu, ikiwa ni pamoja na hangari za ndege za kivita za F35 kwenye kambi ya anga na kituo cha amri na udhibiti cha jeshi la mauaji ya watoto la Marekani huko Al-Azraq, nchini Jordan, kwa makombora ya fueli mango ya masafa marefu.
Taarifa ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ambayo imeanza kwa Aya ya 194 ya Suratul Baqara inayosema: “Na anayekushambulieni nanyi mshambulieni, kwa kadiri alivyokuchokozeni”, imesema: Vikosi vyetu viko tayari kutoa majibu makali zaidi kwa uchokozi wowote mpya kutoka kwa adui, na matokeo ya uchokozi mpya yatakuwa jukumu la adui Mmarekani.
Saa nane na nusu usiku wa kuamkia leo pia, Jeshi la Wanamaji la IRGC lilifanya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kwenye makao makuu ya Kikosi cha Tano cha Wanamaji cha jesi la Marekani nchini Bahrain na katika kambi ya jeshi la Marekani ya Ali al Salem huko Kuwait.
Kabla ya hapo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi alikuwa ameionya Marekani kwamba mashambulizi yake katika maeneo ya kusini mwa Iran “hayatapita bila majibu.”
Sayyid Araqchi alitoa matamshi hayo katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijami wa X baada ya Marekani kushambulia maeneo kadhaa katika Mkoa wa Hormozgan.
“Licha ya kushindwa kwake kwenye uwanja wa vita, Marekani imeamua kujaribu azma yetu,” ameandika Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, akionya kwamba vikosi vya jeshi la Iran “havitaacha shambulio au tishio lolote bila jibu.”
“Ondoka katika eneo letu ikiwa unataka kuwa salama,” amesema Sayyid Abbas Araqchi na kuongeza kwamba: “historia ya Ghuba ya Uajemi ina kurasa nyingi kuhusu hatima mbaya za wageni wanaoingia hapo.”