Jeshi la Jordan limesema leo Jumatano asubuhi kwamba limeharibu makombora matano ya Iran yaliyolenga Azraq, ambapo kambi ya Marekani inapatikana. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Tumezuia na kufyatua makombora matano yaliyorushwa kutoka Iran kuelekea Azraq… Hakukuwa na majeruhi au uharibifu wowote wa vifaa,” jeshi limesema. 

Iran imetangaza leo Jumatano kwamba imelenga kambi za Marekani katika Ghuba ili kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya Washington dhidi ya malengo ya Iran kando ya Mlango-Bahari wa Hormuz, katika mvutano mpya baada ya helikopta ya Marekani kuharibiwa, kitendo kilichohusishwa na Tehran.

Mapema, Walinzi wa Mapinduzi wa Iran walisema walilenga “kambi ya jeshi la anga na kituo cha kamandi ya jeshi la Marekani” huko Azraq, Jordan, kulingana na vyombo vya habari vya serikali ya Iran.

Hata hivyo jeshi la Marekani limesema limekamilisha mashambulizi yake ya anga dhidi ya Iran kujibu kuangushwa kwa helikopta yake ambayo Rais Donald Trump amesema ilidunguliwa na Iran

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *