Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza siku ya  Alhamisi, Juni 11, kwamba alifuta mashambulizi yaliyopangwa kwa siku hiyo dhidi ya Iran, akielezea kwamba “makubaliano mazuri sana” yamefikiwa na Tehran, huku akitangaza kwamba yanaweza kusainiwa mapema mishoni mwa wiki hii barani Ulaya. Hata hivyo, Tehran iko makini zaidi, ikisema kwamba “bado haijafikia hitimisho la mwisho kuhusu makubaliano” na Marekani.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani Donald Trump hatimaye siku ya Alhamisi, Juni 11, alitangaza kwamba amefuta mashambulizi mapya dhidi ya Iran. Hapo awali aliahidi “kuishambulia Iran vikali  usiku wa leo” na kukiteka Kisiwa cha Kharg “pamoja na miundombinu mingine ya mafuta” katika siku za usoni. Sasa, rais wa Marekani anatangaza makubaliano yanayowezekana na Iran.

Trump asema Kiongozi Mkuu wa Iran ameidhinisha makubaliano na Marekani

Donald Trump alisema siku ya Alhamisi, Juni 11, kwamba Kiongozi Mkuu wa Iran, Mojtaba Khamenei, ameidhinisha kile ambacho rais wa Marekani alikiita “mkataba wa makubaliano” na Marekani. “Kutokana na ninavyoelewa, jibu ni ndiyo,” alijibu mwandishi wa habari alipomuuliza kama kiongozi wa Iran ameidhinisha makubaliano kati ya Washington na Tehran.

Kwa upande wake, Iran, kupitia msemaji wake wa Wizara ya Mambo ya Nje, ilisema kwamba bado haijaamua kama iko tayari kusaini makubaliano yaliyotangazwa na Donald Trump ili kukomesha vita.

Iran haijaidhinisha maandishi yoyote ya makubaliano na Washington, kulingana na vyombo vya habari vya serikali ya Iran

Shirika la habari la Iran FARS, likinukuu chanzo kisichojulikana, liliripoti siku ya Alhamisi, Juni 11, kwamba Tehran haijaidhinisha maandishi yoyote kuhusu makubaliano yanayowezekana na Marekani. “Hakuna maandishi yaliyoidhinishwa kwa ajili ya mkataba wa awali wa makubaliano na Marekani,” FARS iliandika, ikinukuu chanzo kilichoelezwa kuwa na taarifa nzuri na karibu na timu ya mazungumzo ya Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *