Kufuatia sintofahamu iliyokuwa inaendelea kwa wakazi na watumiaji wa njia zilizopo Katika nyumba za shirika la nyumba za mtaa wa Fire na Mazengo wilaya ya Ilala jijini DSM, baada ya baadhi ya wakazi wa eneo hilo kuziba njia zilizopo katika mitaa hiyo jambo ambalo lilisababisha sintofahamu kubwa kwa wakazi kupishana na kauli na kuleta uhasama baina yao, Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amefanya ziara ya kwenda kujionea utata wa eneo hilo na kuzungumza na mamia ya wakazi wa mtaa hiyo na kusikiliza pande zote mbili zinazokinzana juu ya kuwekwa mageti katika mitaa.
Baada ya kusikiliza pande zote mbili Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo amewataka wakazi wa eneo hilo kuwa watulivu na kuishi kwa umoja na usalama huku akitoa wiki kukutana na wahusika wote ili kutatua kero hiyo
(Feed generated with FetchRSS)