#HABARI: Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, amewataka wananchi wa Wilaya ya Serengeti na Mkoa wa Mara kwa ujumla kuwa mstari wa mbele katika kulinda amani na usalama wa nchi, akisisitiza kuwa ulinzi na usalama wa taifa hauhusiani na chama cha siasa, dini wala kabila.

Dkt. Nyansaho ametoa kauli hiyo leo wilayani Serengeti mkoani Mara wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Akimkaribisha Waziri Mkuu katika eneo hilo, Dkt. Nyansaho amesema Serengeti inapaswa kuwa mfano wa kudumisha amani, akieleza kuwa eneo hilo ni nyumbani kwake na hivyo linapaswa kuwa chanzo cha mshikamano na utulivu.

Amesema kuaminiwa na Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuongoza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa akiwa mzaliwa wa Serengeti, ni heshima kubwa inayoweka wajibu kwa wananchi wa eneo hilo kuwa vinara wa kulinda amani ya taifa.

Dkt. Nyansaho amesisitiza kuwa ulinzi na usalama wa taifa ni jukumu la kila Mtanzania bila kujali tofauti za kisiasa, kidini au kikabila.

Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
‎Follow ITV TANZANIA RadioOne Tanzania
‎Capitalradio Tanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *