Safari mpya za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kati ya Tanzania na Urusi zimeanza kupata mwitikio mkubwa wa abiria, hatua inayotarajiwa kuongeza idadi ya watalii na kuimarisha biashara kati ya nchi hizo mbili.
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuiimarisha ATCL katika soko hilo, akieleza kuwa mwitikio wa wasafiri kutoka Urusi kuja Tanzania na kutoka Tanzania kwenda Urusi unaonyesha fursa kubwa ya kukuza usafiri wa anga.
Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema njia hiyo mpya itachochea ukuaji wa sekta ya utalii, huku Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Peter Ulanga, akisema shirika hilo limejipanga kutumia fursa hiyo kupanua huduma na kuongeza ushindani katika soko la kimataifa.
✍ Upendo Michael
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)