#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia Beatrice Gabriel Urassa (59), kwa tuhuma za mauaji ya watu wanne ambao walifariki dunia kwa nyakati tofauti wakiwa wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Machame na hospitali ya Wilaya ya Hai.
Waliofariki dunia ni Hamida Hamis Kweka (26), Robson Edson Meena (34), Ismail Exaud Uronu (34) na Kamama Exaud Uronu (45) wote wakazi wa kitongoji cha kinyaro, kata ya Mnadani, wilaya ya Hai na Mkoa wa Kilimanjaro.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa, mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwapatia dawa za kienyeji watu hao ambao ni ndugu wa familia moja, na kupelekea kufariki dunia wakiwa wanapatiwa matibabu Julai 05, 2026 majira ya usiku.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linaendelea na uchunguzi kuhusina na tukio hili, pindi utakapokamilika taratibu nyingine za kisheria zitafuata.
Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)