Iran imedai kuidungua na kuharibu ndege isiyo na rubani ya Marekani aina ya MQ-9 iliyokuwa ikiruka juu ya mji wa Andimeshk.

Kwa mujibu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), ndege hiyo ilidunguliwa kwa kutumia mfumo wa kisasa wa ulinzi wa anga. Hata hivyo, shirika la habari la Tasnim halijawasilisha ushahidi wa kuthibitisha madai hayo.

Hadi sasa, Marekani pamoja na Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM) hawajathibitisha rasmi taarifa hizo.

Je, unaamini madai ya Iran kuhusu kuidungua ndege hiyo ya MQ-9? Tuambie maoni yako kwenye sehemu ya maoni.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *