Kiungo Mshambuliaji Raia wa Afrika Kusini, Skudu Makudubela, ametangaza rasmi kustaafu soka la kulipwa baada ya safari ya miaka 17 iliyojaa mafanikio ndani na nje ya bara la Afrika.

Makudubela amesema alianza safari yake mwaka 2004 kupitia SAFA Transnet School of Excellence, kabla ya kucheza katika klabu mbalimbali za Afrika Kusini, Jamhuri ya Czech, Georgia, Tanzania, DR Congo na Angola.

Katika ujumbe wake wa kuaga, amezishukuru klabu zote alizowahi kuzitumikia, makocha, wachezaji wenzake, madaktari, wahudumu wa vifaa pamoja na mashabiki waliomuunga mkono katika maisha yake yote ya soka.

Amesema atajivunia mataji aliyoyashinda, yakiwemo MTN8, Telkom Cup na NBC Premier League akiwa na Young Africans SC, akisisitiza kuwa soka limemjenga kwa kumpa nidhamu, undugu na upendo ambao ataubeba maisha yake yote.

“Football gave me everything. The discipline. The brotherhood. The love.” – Skudu Makudubela.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *