Iran imesema imefanya mashambulizi mapya dhidi ya kambi za kijeshi za Marekani katika mataifa ya Ghuba, ikiwemo Jordan, Kuwait na Bahrain, huku Marekani nayo ikiendelea kushambulia maeneo ya kijeshi nchini Iran.
Kwa mujibu wa Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM), mashambulizi hayo yalilenga mifumo ya ulinzi wa anga na vituo vya ufuatiliaji wa pwani ili kupunguza uwezo wa Iran kutishia usafiri wa baharini katika Mlango wa Hormuz.
Hatua hiyo imekuja baada ya Rais Donald Trump kuionya Iran kurejea kwenye mazungumzo, huku Tehran ikisisitiza kuwa haitazingatia makubaliano yasiyo na manufaa kwa taifa hilo.
Unaonaje mzozo huu unaoendelea kati ya Marekani na Iran? Je, unaamini utamalizika kwa mazungumzo au utaendelea kuongezeka Tuambie maoni yako kwenye sehemu ya maoni.
#chanzobbcswahili

(Feed generated with FetchRSS)