#TANGAZO: Magonjwa sugu yasiyoambukiza, hususan ugonjwa wa figo, yanaendelea kuwa tishio kwa afya ya Watanzania, huku kisukari na shinikizo la damu vikitajwa kuwa miongoni mwa visababishi vikuu. Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya za mwaka 2023, takribani asilimia saba (7%) ya Watanzania wanaishi na ugonjwa wa figo, hali inayoonesha umuhimu wa kuimarisha huduma za kinga, uchunguzi na matibabu ya magonjwa hayo.
Licha ya jitihada za Serikali za kusogeza huduma za afya karibu na wananchi, mahitaji ya huduma za magonjwa sugu yasiyoambukiza yanaendelea kuongezeka. Hali hiyo imeifanya sekta binafsi kuwa mshirika muhimu katika kuongeza upatikanaji wa huduma za kibingwa, vifaa tiba na teknolojia za kisasa zinazosaidia kuokoa maisha ya wagonjwa.
Akizungumza kuhusu mchango wa sekta binafsi katika kukabiliana na magonjwa hayo, Daktari Bingwa wa Hospitali ya KITONKA Medical Hospital ya jijini Dar es Salaam, Dkt. Rashidi Salim, amesema hospitali hiyo imejikita katika kutoa huduma za kibingwa za magonjwa ya figo kupitia uwepo wa Daktari Bingwa wa Figo (Nephrologist) pamoja na huduma za kusafisha damu (Dialysis). Amesema hospitali inaendelea kuongeza mashine za dialysis ili kukidhi ongezeko la mahitaji ya wagonjwa.
Mbali na huduma za figo, Dkt. Rashidi amesema hospitali imewekeza katika vifaa vya kisasa vya uchunguzi ikiwemo CT Scan, X-ray na Ultrasound, huku huduma ya MRI ikitarajiwa kuanza mara baada ya kukamilika kwa ufungaji wa mashine husika. Ameeleza kuwa uwekezaji huo unalenga kuboresha usahihi wa uchunguzi na kuwezesha wagonjwa kupata matibabu ya magonjwa sugu yasiyoambukizwa.
“Tunaamini kinga ni bora kuliko tiba. Ndiyo maana tunaendelea kuhamasisha wananchi kushiriki katika kambi za afya na kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kugundua magonjwa mapema na kuongeza nafasi ya matibabu kufanikiwa,” amesema Dkt. Rashidi.
Mbali na huduma za figo, KITONKA Medical Hospital pia inatoa huduma mbalimbali za kibingwa zikiwemo matibabu ya mifupa na majeraha, magonjwa ya ndani, upasuaji wa kibingwa, magonjwa ya mfumo wa mkojo, afya ya uzazi kwa wanaume na wanawake, wajawazito, watoto, macho na meno. Kupitia uwekezaji huo,
(Feed generated with FetchRSS)