Zaidi ya huduma 22,000 za matibabu zimetolewa kupitia kambi ya matibabu bila alipo iliyohitimishwa mkoani Arusha, huku mamia ya wananchi wakigundulika kuwa na magonjwa mbalimbali ambayo hawakuwa wakiyafahamu.
Akizungumza baada ya kufungwa kwa kambi hiyo, Mbunge wa Arusha Mjini, Paul makonda amesema wananchi 503 walibainika kuwa na kisukari bila kujua, huku watu 18 waliopimwa saratani wakikutwa na dalili za ugonjwa huo na kuanza kufuatiliwa kwa matibabu ya mapema.
Amesema uchunguzi uliofanywa na madaktari bingwa pia uliwawezesha wananchi wengi kubainika kuwa na matatizo ya moyo, figo na magonjwa mengine, hatua inayoongeza nafasi ya kupata matibabu kwa wakati na kupunguza madhara ya kiafya.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)