Jeshi la Marekani limekiri Jumapili kwamba askari wake mwingine ameuawa kufuatia shambulio la ndege isiyo na rubani ya Iran, huku operesheni za kulipiza kisasi za Jamhuri ya Kiislamu zikiendelea kuwasababishia hasara kubwa askari wa jeshi katili Marekani katika kanda nzima.

Kifo hiki kinakuja siku moja baada ya Wizara ya Vita ya Marekani, Pentagon, kutangaza vifo vya wanajeshi wake wawili nchini Jordan mnamo Julai 17 katika mashambulio ya makombora ya balestiki na ndege zisizo na rubani za Iran.

Mashambulio hayo ya makombora ya balestiki na ndege zisizo na rubani za Iran pia yalimfanya mwanajeshi mwingine wa Marekani kupotea nchini Jordan mnamo Julai 17.

Maafisa wa Marekani walithibitisha Jumapili kupatikana kwa mabaki ya binadamu ambayo bado hayajatambuliwa katika eneo la Jordan, huku uchunguzi ukiendelea kubaini ikiwa ni ya askari huyo aliyepotea. Aidha askari kadhaa walijeruhiwa katika mashambulio hayo.

Matukio haya yanaashiria kupanda kwa kasi kwa gharama ambazo Washington inalazimika kulipa kutokana na uwepo wake wa kijeshi haramu na sera zake za kichokozi katika eneo la Asia Magharibi.

Vikosi vya Iran, kupitia uwezo wa hali ya juu wa ndege zisizo na rubani na makombora, vimeonyesha uwezo wao wa kulenga na kudhoofisha vituo vya majeshi ya Marekani na washirika wake katika eneo.

Wanajeshi wasiopungua 16 wa Marekani wameuawa tangu Februari mwaka wakati utawala huo ulipoanzisha vita dhidi ya Iran kwa kushirikiana na utawala katili wa Israel.

 Ripoti zinaonyesha kuwa mamia ya wanajeshi wa Marekani pia wamejeruhiwa katika vita hivi, na maafisa wa Pentagon wanasita kutoa idadi halisi ya hasara vitani kutokana na hofu ya ghadhabu za umma na kuvunjika kwa moyo miongoni mwa wanajeshi wao.

Wakati huo huo Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kutekeleza shambulio la kushtukiza la kulipiza kisasi dhidi ya kituo cha kamandi ya operesheni maalum za Marekani katika eneo la Al-Tanf nchini Syria, likitoa ujumbe wa wazi kwa utawala katili wa Marekani ambao mikono yake imejaa damu ya watoto.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, katika kulipiza kisasi cha moja kwa moja kwa ajili ya damu ya askari wa Iran waliouawa shahidi siku chache zilizopita katika eneo la Iranshahr.

Taarifa hiyo ya IRGC imesisitiza zaidi udhibiti imara wa Iran juu ya Lango Bahari la Hormuz. Imetangaza kuwa udhibiti kamili wa njia hii muhimu ya maji unasalia mikononi mwa wapiganaji shupavu wa IRGC.

Aidha IRGC imesisitiza kuwa muda wote ambao Marekani itaendeleza uovu wake, uchokozi, na vitendo vya uadui, hakuna tone moja la mafuta au gesi litakalosafirishwa kutoka eneo hilo kupitia njia hii muhimu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *