Dar es Salaam. Mchezaji wa gofu Enosh Wanyeche kutoka klabu ya Lugalo, anasimulia namna ndugu zake walivyokuwa na mchango mkubwa katika kuupenda mchezo huo na kufikia kiwango cha kunyakua baadhi ya mataji makubwa.

Enosh ndiye Tanzania One wa mwaka 2026 kwa wachezaji wa gofu wa amacha ana handicap +3, anaelezea kuwa alianza kwa kuwabebea mabegi ya vifaa vya gofu (kedi) ndugu zake wa damu ambao ni Isaac na Hawa, baadaye wakamshawishi na sasa ni mchezaji mkubwa.

Anasema alianza kucheza kwa ushindani rasmi mwaka 2024 hadi kufanikiwa kuwa Tanzania One, anaona ni hatua kubwa katika maisha yake.

“Mwaka 2025 Tanzania One alikuwa Isihaka Daudi na sasa anashika namba mbili, wote tupo klabu ya Lugalo, namba tatu ni Jay Nathwani kutoka Arusha Gymkhana na Victor Joseph wa Dar Gymkhana,” anasema na kuongeza;

“Victor ni mchezaji mzuri sana, kipindi cha nyuma kabla ya kuondoka nchini na kurejea ndiye alikuwa Tanzania One, akaja Isihaka na sasa mimi, ameshika nafasi ya nne kwa ubora nchini baada ya hivi karibuni kushinda Tanzania Amateur Stroke Play, mshindi wa pili alikuwa Isihaka, mimi nilishika nafasi ya tatu, unaweza ukapata picha ya mchuano wa ushindani baina yetu.”

Anasema kwa sasa kaka yake Isaac ndiye kocha anayemfundisha ingawa ana walimu wengine kutoka nchini Afrika Kusini, wanaomsaidia kumjenga pale anapoona anapwaya.

Kati ya mataji aliyowahi kuyatwaa katika gofu ni la NMB CDF 2024 lililofanyika kwenye mashindano ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliyofanyika Lugalo jijini Dar es Salaam, lingine ni la Lina Professional Golfers (PG) Tour Pro-Am 2024 lililofanyika katika klabu ya Moshi Gymkhana mkoani Kilimanjaro.

“Gofu imebadilisha maisha yangu kwa asilimia kubwa, nimetembea nchini ambazo sikuzitarajia, nimetengeneza koneksheni na watu wengi, maana ili ufanikiwe katika maisha lazima uwe na koneksheni ya watu, ambao unatakiwa kujua ninaweza nikawatumia kwa wakati gani na sababu gani,” anasema na kuongeza;

“Nawashauri vijana wasiogope kuthubutu kujifunza mchezo wa gofu, kama wengi wao walivyojikita katika mpira wa miguu, ngumi, mpira wa kikapu na michezo mingine.

“Wengi wao wakisikia gofu moja kwa moja wanaona ni mchezo unaostahili kuchezwa na matajiri, mimi si tajiri, kila kitu kinahitaji uthubutu, ndiyo maana nilianza kwa kuwasindikiza ndugu zangu nikiwabebea mabegi katika mazoezi na mashindano na sasa ni mchezaji mkubwa kama ilivyo kwa wengine.”

Anasema anaamini kuna siku Tanzania itatoa wanagofu wakubwa:”Kuna wachezaji wakubwa duniani na matajiri, naamini kabisa itafikia huko kwa wadogo zetu wanaojengwa katika misingi mizuri.

Anaongeza:”Kama ambavyo katika mpira wa miguu Mtanzania, Mbwana Samatta alikuwa anaimbwa kila kona wakati anacheza kwa ushindani wa juu nje, ndivyo tunavyotamani iwe inaimbwa kwa wachezaji wa gofu wanaofanya vizu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *