Hispania ndio mabingwa wapya wa kombe la dunia katika mchezo wa soka, baada ya kuifunga waliokuwa mabingwa watetezi Argentina 1-0 katika mechi ya fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa MetLife huko New Jersey nchini Marekani.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Huu ni ubingwa wa kihistoria kwa Hispania, ambayo sasa imeshinda taji hili kwa mara ya pili, baada ya kuibuka washindi kwa mara ya kwanza, mwaka 2010.
Miamba hawa wa soka barani Ulaya, sasa ni mabingwa wa soka dunia, katika mchezo uliochezwa hadi katika muda wa ziada, ambapo dakika ya 106 mshambuliaji wa Ferran Torres, alifunga bao pekee lililoipa ushindi timu yake.
Rais wa Marekani Donald Trump, alikuwa miongoni mwa mashabiki zaidi ya 80,000 walioshuhudia fainali hiyo, ambayo mchezaji wa Argentina‘ Enzo Fernandez alioneshwa kadi nyekundu, na kuiacha timu yake na mlima mkubwa wa wachezaji 10 katika dakika ya 93 ya mchezo.
Baada ya ushindi huo, mamilioni ya raia wa Hispania, wanatarajiwa kuwakaribisha wachezaji wa Hispania, siku ya Jumatatu, ambapo watapita na kombe katikati ya jiji la Madrid na kukutana na Waziri Mkuu Pedro Sanchez.