
Polisi nchini Burundi wamethibitisha kufariki kwa watu wasiopungua wanane katika tukio la mkanyagano wakati wa mkutano wa kidini Jijini Bujumbura.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Vifo hivyo vimetokea baada ya maelfu ya watu kuhudhuria mkutano wa muhubiri maarufu Chris Ndikumana ambaye mtando wake wa Youtube una zaidi wa wafuasi milioni moja.
Kulingana na mashuhuda, tukio hilo lilitokea wakati waumini hao walipotaka kuondoka kwa wakati mmoja baada ya mkutano huo kukamilika, hali iliopelekea mkanyagano huo.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, mbali na vifo hivyo, waumini wengine tisa walijeruhiwa, hata hivyo waandaji wa mkutano huo hawajatoa tamko loloto kuhusu taafira ya vifo na majeruhi.
Makanisa ya kievanjelisti yameendelea kuongezeka kwa kasi barani Afrika huku matukio ya mikanyagano yakishuhudiwa katika mikutano kadhaa mikubwa ya kidini katika miaka ya hivi karibuni.
Katika taifa Jirani la Tanzania, watu takriban 20 walifariki mwaka wa 2020 wakati waking’ang’ania kufikia mafuta takatifu katika mkutano wa kidini wa mhubiri maarufu.