
Jumla ya watu 144 walifariki au kutoweka baharini wiki iliyopita pwani ya Mauritania, Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) limeripoti leo Jumanne, Julai 21, 2026.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Boti hilo iliokolewa mnamo Julai 18 “baada ya kusafiri kwa karibu siku 25 katika Bahari ya Atlantiki. Boti iliondoka Bufalo, Gambia, ikitarajia kufika Uhispania.”
“Kulingana na taarifa zilizokusanywa, watu 143 walifariki au hawajulikani walipo, na ni 38 pekee walionusurika,” msemaji wa UNHCR Matthew Saltmarsh amewaambia waandishi wa habari huko Geneva, akiongeza kuwa kifo kingine kimoja “kiliripotiwa miongoni mwa abiria wa boti iliyotua Julai 14” nchini Mauritania.